DCP Enhanced OCR

Chaguo hili hukuruhusu kufikia huduma za ziada kwenye Document Capture Pro. Kwa kununua leseni, unaweza kufikia vipengele vifuatavyo.

Angalia msaada wa Document Capture Pro ili upate maelezo.

Kumbuka:

DCP Enhanced OCR haikubali Windows Server na Mac OS.

  • Umbizo za ziada za kuhifadhi:

    Unaweza kuteua Microsoft® Word, Microsoft®Excel® na Microsoft® PowerPoint® kama umbizo wa faili.

  • Kipengele cha ubadilishaji wa ubora wa juu (PDF Inayoweza Kutafutwa):

    Unaweza kufikia vipengele vya ubadilishaji wa ubora wa juu ukitumia PDF zinazoweza kutafutwa.

  • Violezo vya ziada vilivyobainishwa na mtumiaji:

    Unaweza kuunda kiolezo kilichobainishwa na mtumiaji unapounda kazi. Unaweza kuweka kiolezo kilichobainishwa na mtumiaji kulingana na misimbo wa upau au OCR, na kuitoa kama data ya kiolezo.

  • Chaguo za ziada za kutoa vipengee vya kiolezo:

    Machaguo yafuatayo huongezwa kwenye mipangilio ya kiolezo wakati wa kuunda kazi.

    • Index Separation > Document

      Unaweza kuhifadhi kiolezo katika vitengo vya faili ya picha ili itolewe.

    • File Name > File Name

      Unaweza pia kuongeza jina la faili la picha iliyochanganuliwa kwenye faili ya kiolezo.