Dokezo la Unapotumia Muunganisho wa Wi-Fi 5 GHz

Kichapishi hiki mara nyingi hutumia W52 (36ch) kama kituo unapounganisha kwenye Wi-Fi Direct (AP Rahisi). Kwa kuwa kituo cha muunganisho wa LAN (Wi-Fi) ya pasiwaya kimeteuliwa otomatiki, kituo kilichotumika kinaweza kuwa tofauti kwa wakati sawa na muunganisho wa Wi-Fi Direct. Kutuma data kwa kichapishi kunaweza kucheleweshwa iwapo vituo ni tofauti. Iwapo haiingiliani na matumizi, unganisha kwenye SSID katika bendi ya 2.4 GHz. Katika bendi ya 2.4 GHz, vituo vilivyotumika vitalingana.

Unapoweka LAN ya pasiwaya kwa 5 GHz,tunapendekeza kulemaza Wi-Fi Direct.