Iwapo utagundua mistari wima isiyopangwa vizuri, taswira zisizoonekana vizuri, au mistari mlalo inayoonekana kwa umbali, rekebisha ubora wa chapisho. Iwapo unataka kurekebisha ubora wa chapisho kwa karatasi, kwanza unda mpangilio huu. Thamani ya mpangilio kwa karatasi inawekwa upya iwapo utaunda mpangilio huu baada ya kurekebisha kwa karatasi.
Weka karatasi tupu yenye ukubwa wa A4 katika kichapishi.
Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya
, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.
Teua Urekebishaji wa Ubora wa Chapa.
Fuata maagizo kwenye skrini ili kuchapisha ruwaza ya mpangilio wa kichwa cha chapisho, na kisha pangilia kichwa cha kuchapisha.


