> Kunakili > Mbinu Zinazopatikana za Kunakili > Kunakili Nakala asili Anuwai kwenye Laha Moja

Kunakili Nakala asili Anuwai kwenye Laha Moja

Unaweza kunakili nakala asili anuwai kwenye laha moja la karatasi.

  1. Weka nakala zote asili zikiwa zinaangalia juu katika ADF.

    Kuweka Nakala Asili

    Ziweke katika mwelekeo ulioonyeshwa kwenye mfano.

    • Nakala asili za Taswira
    • Nakala asili la Mandhari
    Muhimu:

    Iwapo unataka kunakili nakala asili ambazo haziauniwi na ADF, tumia glasi ya kitambazaji.

    Nakala asili ambazo Haziauniwi na ADF

    Kumbuka:

    Pia unaweza kuweka nakala asili kwenye glasi ya kitambazaji.

    Kuweka Nakala Asili

  2. Teua Nakili kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Teua kichupo cha Mipangilio Mahiri, na kisha uteue Kurasa Nyingi > 2-juu.

  4. Bainisha mpangilio wa muundo na mwelekeo, na kisha uteue Sawa.

  5. Bonyeza kitufe cha .