Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kiotomatiki kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya. Ikiwa masharti yafuatayo yatatimizwa, unaweza kusanidi kwa kutumia mbinu hii.
Kipanga njia pasiwaya kinatangamana na WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa).
Muunganisho wa sasa wa Wi-Fi ulitambuliwa kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya.
Teua
kwenye skrini ya nyumbani.
Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya
, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).
Iwapo tayari kichapishi kimeunganishwa na Ethaneti, teua Kipangishi njia.
Bonyeza kitufe cha OK.
Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Teua Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.
Iwapo kichapishi tauari kimeunganishwa kwa Ethaneti, teua Badilisha kwa muunganisho wa Wi-Fi., na kisha uteue Ndiyo baada ya kuangalia ujumbe.
Teua Sukuma Kitufe cha Usanidi (WPS).
Shikilia chini kitufe cha [WPS] kwenye kipanga njia pasiwaya hadi taa ya usalama imweke.

Ikiwa hujui kilipo kitufe cha [WPS], au hakuna vitufe kwenye kipanga njia pasiwaya, tazama hati iliyotolewa yenye kipamnga njia pasiwaya kwa maelezo.
Bonyeza kitufe cha OK kwenye kichapishi.
Funga skrini.
Skrini hufunga kiotomatiki baada ya kipindi maalum cha muda.
Iwapo muunganisho utashindikana, washa upya kipanmga njia pasiwaya, kisogeze karibu na kichapishi, na ujaribu tena. Iwapo haitafanya kazi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na uangalie suluhisho.
Bonyeza kitufe cha
.