> Utambazaji > Kutambaza Nakala Asili kwenye Kompyuta > Kutambaza Kutoka kwa Paneli Dhibiti

Kutambaza Kutoka kwa Paneli Dhibiti

Kumbuka:

Ili kutumia kipengele hiki, hakikisha kwamba programu zifuatazo zimesakinishwa kwenye kompyuta yako.

  • Epson ScanSmart (Windows 7 au la naadaye, au OS X El Capitan au la baadaye)

  • Epson Event Manager (Windows Vista/Windows XP, au OS X Yosemite/OS X Mavericks/OS X Mountain Lion/Mac OS X v10.7.x/Mac OS X v10.6.8)

  • Epson Scan 2 (programu zinazohitajika ili utumie kipengele cha kitambazaji)

Tazama yafuatayo ili uangalie ikiwa kuna programu za kusakinisha.

Windows 10: bofya kwenye kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Mifumo ya WindowsPaneli DhibitiProgramuProgramu na Vipengele.

Windows 8.1/Windows 8: teua Eneo-KaziMipangilioPaneli DhibitiProgramuProgramu na Vipengele.

Windows 7/Windowes Vista: bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Paneli DhibitiProgramuProgramu na Vipengele.

Windows XP: bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Paneli Dhibiti-Ongeza au Ondoa Programu.

Mac OS: teua Nenda > Programu > Epson Software.

  1. Weka nakala za kwanza.

    Kuweka Nakala Asili

  2. Teua Changanua > Kompyuta kwenye paneli dhibiti.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Chagua kompyuta ya kuhifadhi picha zilizotambazwa.

    • Ikiwa skrini ya Chagua Kompyuta imeonyeshwa, teua kompyuta kutoka kwenye skrini.
    • Iwapo skrini ya Tambaza kwenye Kompyuta imeonyeshwa na kompyuta tayari imeteuliwa, hakikisha kompyuta iliyoteuliwa ni sahihi. Iwapo unataka kubadilisha kompyuta, teua , kisha uteue kompyuta nyingine.
  4. Teua ili kuteua jinsi ya kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta.

    • Hakiki kwenye Kompyuta (Windows 7 au la baadaye, au OS X El Capitan au la baadaye): hakiki taswira iliyotambazwa kwenye kopmyuta kabla ya kuhifadhi taswira.
    • Hifadhi kama JPEG: huhifadhi picha iliyotambazwa kwenye umbizo la JPEG.
    • Hifadhi kama PDF: huhifadhi picha iliyotambazwa kwenye umbizo la PDF.
  5. Bonyeza kitufe cha .

Unapotumia Windows 7 au la baadaye, au OS X El Capitan au la baadaye: Epson ScanSmart huwashwa kiotomatiki kwenye kompyuta yako, na utambazaji huanza.

Kumbuka:

Tazama usaidizi wa Epson ScanSmart kwa taarifa kamili ya kutumia programu. Bofya Help kwenye skrini ya Epson ScanSmart ili kufungua msaada.