Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kwa kuingiza maelezo muhimu ya kuunganisha kwenye kipanga njia pasiwaya kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Ili kusanidi kwa kutumia mbinu hii, unahitaji SSID na nenosiri kwa kipanga njia pasiwaya.
Iwapo unatumia eneo la kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio yake chaguo-msingi, SSID na nywila ziko kwenye lebo. Iwapo hufahamu SSID na nywila, tazama nyaraka zilizotolewa na kipanga njia pasiwaya.

Teua
kwenye skrini ya nyumbani.
Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya
, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).
Iwapo tayari kichapishi kimeunganishwa na Ethaneti, teua Kipangishi njia.
Bonyeza kitufe cha OK ili kuonyesha skrini inayofuata.
Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Teua Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.
Iwapo kichapishi tauari kimeunganishwa kwa Ethaneti, teua Badilisha kwa muunganisho wa Wi-Fi., na kisha uteue Ndiyo baada ya kuangalia ujumbe.
Teua Sogora ya Kusanidi Wi-Fi.
Teua SSID kwa kipanga njia pasiwaya.
Iwapo SSID unayotaka kuunganisha kwayo haionyeshwi kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, bonyeza
ili kusasisha orodha. Iwapo bado haitaonyeshwa, teua
, na kisha uingize SSID moja kwa moja.
Iwapo hujui jina la mtandao (SSID) angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Iwapo unatumia kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio yake chaguo-msingi, tumia SSID kwenye lebo. Iwapo huwezi kutafuta maelezo yoyote, tazama nyaraka zilizotolewa pamoja na kipanga njia pasiwaya.
Bonyeza kitufe cha Sawa, na kisha uingize nenosiri.
Nenosiri linaathiriwa na herufi kubwa au ndogo.
Iwapo hujui nenosiri, angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Kwenye lebo, nenosiri linaweza kuandikwa “Network Key”, “Wireless Password”, na kadhalika. Ikiwa unatumia kipanga njia pasiwaya na mipangilio yake chaguomsingi, tumia nenosiri lilioandikwa kwenye lebo.
Unapokamilisha, teua OK.
Angalia mipangilio, na kisha uteue Anza Kusanidi.
Funga skrini.
Skrini hufunga kiotomatiki baada ya kipindi maalum cha muda.
Ukishindwa kuunganisha, pakia karatasi tupu la ukubwa wa A4, na kisha uteue Chapisha Ripoti ya Ukaguzi ili kuchapisha ripoti ya muunganisho.
Bonyeza kitufe cha
.