> Kuchapisha > Kuchapisha Nyaraka > Kuchapisha Nyaraka kutoka Vifaa Maizi (Android) > Kuchapisha Nyaraka kwa kutumia Epson Print Enabler

Kuchapisha Nyaraka kwa kutumia Epson Print Enabler

Unaweza kuchapisha hati, barua pepe, picha au kurasa za wavuti pasiwaya moja kwa moja kutoka katika simu au kompyuta yako kibao Android (Android v 4.4 au jipya zaidi). Kwa kudonoa mara chache tu, kifaa chako cha Android kinaweza kugundua kichapishi cha Epson ambacho kimeunganishwa kwenye mtandao sawa pasiwaya.

Kumbuka:

Uendeshaji unaweza kutofautiana kulingana na kifaa.

  1. Sanidi kichapishi chako kwa uchapishi wa pasi waya. Tazama kiungo cha hapa chini.

    http://epson.sn

  2. Sakinisha programu-jalizi ya Kiwezeshaji cha Kichapishi cha Epson kutoka kwa Google Play.

  3. Unganisha kifa chako cha Android kwenye mtandao sawa wa pasi waya ambao kichapishi chako kinatumia.

  4. Nenda katika Mipangilio kwenye kifaa cha Android, teua Kuchapisha kisha wezesha Epson Print Enabler.

  5. Kutoka katika programu ya Android kama vile Chrome, donoa aikoni ya menyu na uchapishe kilicho kwenye skrini.

    Kumbuka:

    Iwapo hutaona kichapishi chako, donoa Vichapishi Vyote na uteue kichapishi chako.