> Kukarabati Kichapishi > Kusafisha Wino Uliomwagika

Kusafisha Wino Uliomwagika

Iwapo wino umemwagika, usafishe kwa njia zifuatazo.

  • Iwapo wino utamwagika katika eneo lililo karibu na tangi, pangusa kwa kutumia kitambaa safi laini au pamba.

  • Iwapo wino utamwagika kwenye dawati au sakafuni, upanguse mara moja. Wino unapokauka, itakuwa vigumu kuuondoa. Ili kuzuia ueneaji wa wino, weka kitambaa kwenye wino, na kisha uupanguse kwa kitambaa cha unyenunyevu.

  • Iwapo wino utajipaka kwenye mikono yako, nawa kwa maji na sabuni.