Kuunda Mipangilio ili Kuhifadhi Faksi Zilizopokwa

Kichapishi kimewekwa ili kuchapisha faksi zilizopokewa kwa chaguo-msingi. Kando na kuchapisha, unaweza kuweka kichapishi kuhifadhi faksi zilizopokewa.

  • Kisanduku pokezi kwenye Kichapishi

    Unaweza kuhifadhi faksi zilizopokewa kwenye Kisanduku pokezi. Unaweza kuzitazama kwenye paneli dhibiti ya kichapishi ili uweze tu kuchapisha zile amnazpo unataka kuchapisha au kufuta faksi zisizohitajika.

  • Kompyuta (mapokezi ya KOMPYUTA-FAKSI)

Vipengele vilivyo hapa juu vinaweza kutumiwa kwa wakati mmoja. Ukivitumia kwa wakati mmoja, nyaraka zilizopokewa zinahifadhiwa kwenye kisanduku pokezi na kwenye kompyuta. Ili kupokea faksi kwenye kompyuta, unda mipangilio kwa kutumia FAX Utility.

Kuunda Mipangilio ya Kutuma na Kupokea Faksi kwenye Kompyuta

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Faksi Towe.

  3. Iwapo ujumbe wa uthibitisho umeonyeshwa, uthibitishe, na kisha donoa Sawa.

  4. Teua Hifadhi kwenye Kikasha.

  5. Teua Hifadhi kwenye Kikasha ili uweke hii kwenye nafasi ya On

  6. Teua Chaguo wakati kumbukumbu imejaa, teua chaguo ili utumie wakati kisanduku pokezi kimejaa.

    • Pokea na uchapishe faksi: kichapishi huchapisha nyaraka zote zilizopokewa ambazo haziwezi kuhifadhiwa kwenye Kisanduku pokezi.
    • Kataa faksi zinazoingia: kichapishi hakijibu simu zinazoingia za faksi.
  7. Unaweza kuweka nywila ya kisanduku pokezi. Teua Mipang. Nenosiri la Kisanduku pokezi, na kisha uweke nenosiri.

    Kumbuka:

    Huwezi kuweka nenosiri wakati Chaguo wakati kumbukumbu imejaa imewekwa kwa Pokea na uchapishe faksi.