Unapoweka ili kukuarifu kuwepo kwa faksi mpya, dirisha la taarifa linaonyeshwa karibu na mwambaa wa kazi kwa kila faksi.
Angalia skrini ya taarifa inayoonyeshwa kwenye skrini yako ya kompyuta.
Skrini ya taarifa hutoweka iwapo hakuna operesheni inayotekelezwa kwa kipindi fulani cha muda. Unaweza kubadilisha mipangilio ya taarifa kama vile muda wa onyesho.
Bofya mahali popote kwenye skrini ya taarifa, isipokuwa kwa kitufe cha .
Skrini ya Receiving Fax Record inaonyeshwa.
Angalia tarehe na mtumaji kwenye orodha, na kisha ufungue faili ya PDF.
Faksi zilizopokewa zinabadilishwa jina kiotomatiki kwa kutumia umbizo lifuatalo la utoaji majina.
YYYYMMDDHHMMSS_xxxxxxxxxx_nnnnn (Mwaka/Mwezi/Siku/Saa/Dakika/Sekunde_nambari ya mtumaji)
Pia unaweza kufungua kabrasha la faksi iliyopokewa moja kwa moja unapobofya ikoni ya kulia. Kwa maelezo, tazama Optional Settings kwenye msaada wa FAX Utility (yanayoonyeshwa kwenye dirisha kuu).