Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi
Mipangilio Msingi
Mwangaza wa LCD
Rekebisha mwangaza wa skrini ya LCD.
Sauti
Rekebisha sauti.
Nyamazisha
Teua On ili kunyamazisha sauti kama zile zitolewazo na Ubonyezaji Kitufe.
Hali ya Kawaida
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe.
Hali Tulivu
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe kwenye Hali Tulivu.
Kipima saa cha Kulala
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Kipima Saa ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Mip'ilio ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha LINE kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Teua mpangilio wa wakati wa majira ya joto unaotumika katika eneo lako.
Utofauti wa Saa
Ingiza tofauti ya saa kati ya saa yako ya ndani na UTC (Saa Inayoratibiwa ya Kimataifa).
Nchi/Eneo
Teua nchi au eneo ambalo unatumia kichapishi chako. Iwapo utabadilisha nchi au eneo, mipangilio yako ya faksi inarejea kwa chaguo-msingi na lazima uiteue tena.
Lugha/Language
Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.
Pazia
Badilisha rangi ya mandharinyuma ya skrini ya nyumbani.
Muda wa Shughuli Umeisha
Teua On ili kurejesha skrini ya kwanza wakati hakuna operesheni imetekelezwa kwa muda uliobainishwa.