Ubainifu huonyesha idadi ya pikseli (eneo ndogo zaidi la picha) kwa kila inchi (25.4 mm), na hupimwa kwa dpi (nukta kwa kila inchi). Manufaa ya kuongeza ubainifu ni kwamba maelezo kwenye taswira yanakuwa shwari. Hata hivyo, inaweza kuwa na matatizo yafuatayo.
Ukubwa wa faili huwa mpana sana
(Unapoweka ubainifu maradufu, ukubwa wa faili unakuwa pana karibu mara nne zaidi.)
Kutambaza, kuhifadhi na kusoma taswira huchukua muda zaidi
Kutuma na kupokea barua pepe au faksi hucuhukua muda zaidi
Tasiwira inakuwa kubwa zaidi na haiwezi kutosha kwenye onyesho au kuchapishwa kwenye karatasi
Angalia jedwali na uweke ubainifu unaofaa kwa madhumuni ya taswira yako iliyotambazwa.
Madhumuni |
Ubainifu (Rejeleo) |
---|---|
Kuonyesha kwenye kompyuta Kutuma kwa barua pepe |
Hadi dpi 200 |
Kuchapisha kwa kutumia kichapishi Kutuma kwa faksi |
dpi 200 hadi 300 |