Unaweza kuboresha uonekanaji wa matini na picha kwenye machapisho.

Chapisho Lote la Rangi kinapatikana tu mipangilio ifuatayo inapoteuliwa.
Aina ya karatasi: Karatasi tupu, Karatasi ya nakala, Kichwa cha barua, Karatasi iliyofanywa upya, Karatasi ya rangi, Karatasi iliyochapishwa mapema, au Karatasi tupu ya ubora wa juu
Ubora: Wastani au ubora wa juu
Rangi ya Kuchapisha: Rangi
Proghramu-tumizi: Microsoft® Office 2007 au toleo la baadaye
Ukubwa wa Matini: Alama 96 au kidogo
Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi cha Chaguo Zaidi, bofya Chaguo za Taswira kwenye mpangilio wa Usahihishaji wa Rangi.
Teua chaguo kutoka kwenye mpangilio wa Chapisho Lote la Rangi.
Chaguo za Uboreshaji ili uunde mipangilio zaidi.
Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.
Bofya Chapisha.
Baadhi ya vibambo vinaweza kubadilishwa kwa ruwaza, kama vile “+”uonekana kama “±”.
Ruwaza na mistari ya chini maalum ya programu-tumizi inaweza kubadilisha maudhui yaliyochapishwa kwa kutumia mipangilio hii.
Ubora wa chapisho unaweza kupungua kwenye picha na taswira nyingine unapotumia mipangilio ya Chapisho Lote la Rangi.
Kasi ya uchapishaji inapungua unapotumia mipangilio ya Chapisho Lote la Rangi.