Ubora wa Taswira ya Faksi Iliyotumwa ni Duni

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Mpangilio wa Aina ya Nakala Asili sio sahihi.

Suluhisho

Teua Faksi > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Utambazaji > Aina Asili, na kisha ubadilishe mpangilio. Iwapo nakala asili unayotuma ina matini na taswira, weka hii iwe Picha.

Mwonekano umewekwa kuwa chini.

Suluhisho

Iwapo hufahamu utendaji wa mashine ya faksi ya mtumaji, weka yafuatayo kabla ya kutuma faksi.

  • Teua Faksi > Mipangilio ya Faksi na kisha uweke mpangilio wa Mwonekano ili uweke taswira ya ubora wa juu zaidi.

  • Teua Faksi > Mipangilio ya Faksi na kisha uwezeshe Tuma Moja kwa Moja.

    Kumbuka kwamba ukiweka Mwonekano iwe Bora Zaidi au Bora Sana lakini utume faksi bila kuwezesha Tuma Moja kwa Moja, faksi inaweza kutumwa kwa ubainifu wa chini.

Mpangilio wa ECM umelemazwa.

Suluhisho

Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi na uwezeshe mpangilio wa ECM kwenye paneli dhibiti. Huenda hii ikaondoa kosa linatokea kwa sababu ya matatizo ya muunganisho. Kumbuka kwamba kasi ya kutuma na kupokea faksi inaweza kuwa ya chini kuliko ECM inapolemazwa.