Unaweza kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili kuangalia hali kati ya kichapishi na kipanga njia pasiwaya.
Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.
Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho.
Ukaguzi wa muunganisho unaanza.
Teua Chapisha Ripoti ya Ukaguzi.
Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Iwapo kosa limetokea, angalia ripoti ya muunganisho, na kisha ufuate suluhisho zilizochapishwa.