Kutumia Web Config au zana nyingine, unaweza kucheleza na kuleta waasiliani.
Kwa Web Config, unaweza kucheleza waasiliani kwa kuhamisha mipangilio ya kichapishi inayojumuisha waasiliani. Faili iliyohamishwa haiwezi kuhaririwa kwa sababu imahamishwa kama faili ya jozi.
Unapoleta mipangilio ya kichapishi kwenye kichapishi, waasiliani wanafutwa.
Kwa Epson Device Admin, waasiliani pekee wanaweza kuhamishwa kutoka kwenye skrini ya mali ya kifaa chako. Pia, iwapo hutahamisha vipengee vinavyohusiana na usalama, unaweza kuhariri waasiliani waliohamishwa na kuwaleta kawa sababu hii inaweza kuhifadhiwa kama faili ya SYLK au CSV.