Kuhamisha Waasiliani

Hifadhi maelezo ya waasiliani kutoka kwenye faili.

Unaweza kuharirifaili zilizohifadhiwa kwenye umbizo la sylk au csv kwa kutumia programu-tumizi ya laha jedwali au kihariri cha matini. Unaweza kusajili zote mara moja baada ya kufuta au kuongeza maelezo.

Maelezo yanayojumuisha vipengee vya usalama kama vile nenosiri na maelezo ya kibinafsi yanaweza kuhifadhiwa kwenye umbizo la jozi kwa nenosiri. Huwezi kuhariri faili. Hii inaweza kutumika kama faili ya chelezo ya maelezo ikijumuisha vipengee vya usalama.

  1. Anzisha Epson Device Admin.

  2. Teua Devices kwenye mwambaa wa kabdo wa menyu ya kazi.

  3. Teua kifaa unachotaka kusanidi kutoka kwenye orodha ya kifaa.

  4. Bofya Device Configuration kwenye kichupo cha Home kwenye menyu ya riboni.

    Wakati nywila yamsimamizi imewekwa, ingiza nywila na ubofye OK.

  5. Bofya Common > Contacts.

  6. Teua umbizo la kuhamisha kutoka kwenye Export >Export items.

    • All Items
      Hamisha faili ya jozi iliyosimbwa fiche. Teua unapotaka kujumuisha vipengee vya usalama kama vile nenosiri na maelezo ya kibinafsi. Huwezi kuhariri faili. Ukiiteua, unafaa kuweka nenosiri. Bofya Configuration na uweke nenosiri kati ya vibambo 8 na 63 kwa urefu kwenye ASCII. Nenosiri hili linahitajika unapoleta faili ya jozi.
    • Items except Security Information
      Hamisha faili za umbizo la sylk au csv. Teua unapotaka kuhariri maelezo ya faili iliyohamishwa.
  7. Bofya Export.

  8. Bainisha eneo la kuhifadhi faili, teua aina ya faili, na kisha ubofye Save.

    Ujumbe wa ukamilisho unaonyeshwa.

  9. Bofya OK.

    Hakikisha kuwa faili imehifadhiwa katika eneo lililobainishwa.