> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Huonyesha skrini ya Hali ya Printa.

Unaweza kuangalia takriban ya maisha ya huduma ya kikasha cha matengenezo.

Huonyesha hali ya muunganisho wa mtandao. Angalia yafuatayo kwa maelezo zaidi.

Mwongozo kwa Aikoni ya Mtandao

Huonyesha skrini ya Mipangilio ya Sauti ya Kifaa.

Unaweza kuweka Nyamazisha na Hali Tulivu. Pia unaweza kufikia menyu ya Sauti kutoka kwenye skrini. Unaweza pia kuweka mipangilio hii kutoka kwenye menyu ya Mipangilio.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Sauti

Huonyesha iwapo Hali Tulivu imewekwa klwa kichapishi au la. Kipengele kinapowezeshwa, kelele iliyopigwa na operesheni za kichapishi inapunguika, lakini kasi ya kuchapisha inaweza kupungua. Hata hivyo, huenda kelele isipungue kwenye aina ya karatasi iliyoteuliwa na ubora wa chapisho.

Huonyesha kuwa Nyamazisha imewekwa kwa kichapishi.

Teua ikoni ili kuingiza modi ya kusinzia. Wakati ikoni imewekewa rangi ya kijivu, kichapishi hakiwezi kuingiza modi ya kusinzia.

Huonyesha kuwa kipengele cha kizuizi cha mtumiaji kimewezeshwa. Teua ikoni hii ili kuingia kwenye kichapishi. Unahitaji kuteua jina la mtumiaji na kisha ingiza nywila. Wasiliana na msimamizi wako wa kichapishi kwa maelezo ya kuingia.

Wakati imeonyeshwa, mtumiaji aliye ya idhini ya ufikiaji ameingia. Teua aikoni ili uondoke.

Huonyesha skrini ya Maelezo ya Data ya Faksi. Nambari inayoonyeshwa inaashiria idadi ya faksi ambazo bado hujasoma, kuchapisha au kuhifadhi.

Huonyesha kila menyu.

  • Nakili

    Hukuruhusu kunakili nyaraka.

  • Changanua

    Hukuruhusu kutambaza nyaraka na kuzihifadhi kwenye kifaa cha kumbukumbu au kompyuta.

  • Faksi

    Hukuruhusu kutuma faksi.

  • Zili'a Kabla

    Hukuruhusu kusajili mipangilio inayotumika mara kwa mara kunakili, kutambaza au kutuma faksi kama uwekaji awali.

  • Kifaa cha Kumbukumbu

    Hukuruhusu kuchapisha data ya JPEG au TIFF kwenye kifaa cha kumbukumbu kama vile kiendeshi cha USB kilichounganishwa kwenye kichapishi.

  • Kasha la Faksi

    Hukuruhusu kuhifadhi hati zilizopokelewa, hati za kutuma au hati kwa ajili ya kutuma faksi.

  • Kazi ya Siri

    Hukuruhusu kuchapisha kazi iliyolindwa kwa nywila iliyotumwa kutoka kwenye kiendesha kichapishi.

  • Mipangilio

    Hukuruhusu kuweka mipangilio inayohusiana na udumishaji, mipangilio ya kichapishi na operesheni.

Kazi/Hali

Huonyesha kazi zinazoendelea zinazosubiri. Donoa ili kuonyesha aina ya kazi, kipima muda wa kuwasili, majina ya mtumiaji, nakadhalika kama orodha. Nambari inayoonyeshwa huashiria idadi ya kazi zinazosubiri.

Husimamisha operesheni ya sasa. Umbo la ikoni hii hutofautiana kiasi isipokuwa wakati imeonyeshwa kwenye skrini ya nyumbani. Ikoni imeonyeshwa kulingana na hali.

Hutelezesha skrini upande wa kulia.