Unaweza kutafuta Kikasha pokezi/Siri kwenye Kasha la Faksi kwenye skrini ya nyumbani.
Kisanduku pokezi na vikasha vya siri kwenye Kasha la Faksi > Kikasha pokezi/Siri.
Unaweza kuhifadhi hadi nyaraka 100 kwenye kikasha pokezi na kikasha cha siri kwa jumla.
Unaweza kutumia Kikasha pokezi kimoja na usajili hadi vikasha 10 vya siri. Jina la kikasha linaonyeshwa kwenye kikasha. Ya siri XX ni jina chaguo-msingi kwa kila kikasha cha siri.
Huonyesha orodha ya faksi zilizopokewa kwa tarehe zilipokewa, jina la mtumaji, na kurasa.
Kudonoa mojawapo ya faksi kutoka kwenye orodha hufungua skrini ya uhakiki, na unaweza kuangalia maudhui ya faksi. Unaweza kuchapisha au kufuta faksi unapohakiki.
: hupunguza au kuongeza.
: huzungusha picha upande wa kulia kwa digrii 90.
: husogeza skrini katika mwelekeo wa vishale.
: husonga kwa ukurasa wa awali au unaofuata.
Ili kuficha ikoni za operesheni, donoa mahali popote kwenye skrini ya uhakiki isipokuwa kwa ikoni. Donoa tena ili kuonyesha ikoni.
(Menyu ya Kasha)
Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huchapisha faksi zote kwenye kikasha. Kuteua On kwenye Futa Ikikamilika hufuta faksi zote wakati uchapishaji umekamilika.
Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huhifadhi faksi zote kwenye vifaa vya kumbukumbu ya nje kwenye kikasha. Kuteua On kwenye Futa Ikikamilika hufuta nyaraka zote wakati kuhifahi kumekamilika.
Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Hufuta faksi zote kwenye kikasha.
Vipengee vifuatavyo vinaonyeshwa unapoteua Kisanduku pokezi > Menyu ya Kasha > Mipangilio.
Chaguo wakati kumbukumbu imejaa: teua chaguo moja ili kuchapisha au kukataa faksi zinazoingia baada ya Kikasha pokezi kujaa.
Mipangilio ya Nenosiri la Kisanduku pokezi: unaweza kuweka nywila au kuibadilisha.
Vipengee vifuatavyo vinaonyeshwa unapoteua kikasha cha siri na kuteua Menyu ya Kasha > Mipangilio.
Jina: ingiza jina la kikasha cha siri.
Nywila ya Kufungua Kikasha: unaweza kuweka nywila au kuibadilisha.