Unaweza kurekebisha rangi zinazotumiwa katika uchapishaji. Marekebisho haya hayatumiwi kwenye data ya kwanza.

Ubora Picha hutoa picha nzuri zaidi na rangi dhahiri zaidi kwa kurekebisha ulinganuaji, ukifishwaji, na uangavu wa data ya kwanza ya picha kiotomatiki.
Ubora Picha hurekebisha rangi kwa kuchanganua eneo la kipengele. Kwa hivyo, ikiwa umebadilisha eneo la kipengele kwa kupunguza, kukuza, kupogoa, au kuzungusha picha hiyo, rangi inaweza kubadilika bila kutarajiwa. Kuteua mipangilio isiyompaka pia hubadilisha eneo la mada na kusababisha kubadilika kwa rangi. Ikiwa picha iko nje ya mwimo, toni inaweza kuwa sio ya kiasili. Ikiwa rangi imebadilishwa au imekuwa sio ya asili, chapisha kwa modi nyingine mbali na Ubora Picha.
Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi cha Chaguo Zaidi, teua mbinu ya ubadilishaji wa rangi kutoka kwenye mpangilio wa Usahihishaji wa Rangi .
Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.
Bofya Chapisha.