Kuangalia Hali Ya Muunganisho

Tumia Epson Printer Connection Checker kuangalia hali ya muunganisho ya kompyuta na kichapishi. Unaweza kutatua tatizo kwa kutegemea matokeo ya uangaliaji.

  1. Donoa aikoni ya Epson Printer Connection Checker mara mbili kwenye eneo-kazi.

    Epson Printer Connection Checker huanza.

    Iwapo hakuna aikoni kwenye eneo-kazi, fuata mbinu zilizo hapa chini ili kuwasha Epson Printer Connection Checker.

    • Windows 10
      Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Epson Software > Epson Printer Connection Checker.
    • Windows 8.1/Windows 8
      Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
    • Windows 7
      Bofya kitufe cha kuwasha kisha uteue Programu Zote > Epson Software > Epson Printer Connection Checker.
  2. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kuangalia.

    Kumbuka:

    Iwapo jina la kichapishi halionyeshwi, sakinisha kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson.

    Kuangalia ikiwa kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson kimesakinishwa — Windows

Ikiwa umetambua tatizo, fuata suluhu inayoonyeshwa kwenye skrini.

Ikiwa huwezi kutatua tatizo, angallia yafuatayo kulingana na hali yako.