Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kwa kuingiza maelezo muhimu ya kuunganisha kwenye kipanga njia pasiwaya kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Ili kusanidi kwa kutumia mbinu hii, unahitaji SSID na nenosiri kwa kipanga njia pasiwaya.
Iwapo unatumia kipamnga njia pasiwaya na mipangilio chaguo-msingi, SSID na nenosiri vipo kwenye lebo. Iwapo hujui SSID na nenosiri, wasiliana na mtu aliyesanidi kipanga njia pasiwaya, au tazama uwekaji nyaraka uliotolewa na kipanga njia pasiwaya.

Donoa
kwenye skrini ya nyumbani.
Teua Kipangishi njia.
Donoa Anza Kusanidi.
Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Donoa Badilisha kwa muunganisho wa Wi-Fi. au Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.
Teua Sogora ya Kusanidi Wi-Fi.
Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuteua SSID, weka nywila ya kipanga njia pasi waya na usanidi.
Ukitaka kuangalia hali ya muunganisho wa mtandao ya kichapishi baada ya kukamilisha kusanidi, angalia kiungo cha maelezo husiani kilicho hapa chini kwa maelezo.
Iwapo hujui SSID, angalia kama imeandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Iwapo unatumia kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio chaguo-msingi, tumia SSID iliyoandikwa kwenye lebo. Iwapo huwezi kutafuta maelezo yoyote, tazama nyaraka zilizotolewa pamoja na kipanga njia pasiwaya.
Nenosiri linaathiriwa na herufi kubwa au ndogo.
Iwapo hujui nenosiri, angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Kwenye lebo, nenosiri linaweza kuandikwa “Network Key”, “Wireless Password”, na kadhalika. Ikiwa unatumia kipanga njia pasiwaya na mipangilio yake chaguomsingi, tumia nenosiri lilioandikwa kwenye lebo.