Ili kutuma na kupokea faksi kwenye kompyuta ya mteja, FAX Utility inafaa kusakinishwa kwenye komnpyuta iliyounganishwa na mtandao au kebo ya USB.
Weka mipangilio ya yafuatayo ukitumia Web Config.
Fikia Web Config, bofya kichupo cha Fax na kisha ubofye Send Settings.
Teua Use kwa ajilil ya PC to FAX Function.
Thamani chaguomsingi ya PC to FAX Function ni Use. Ili kulemaza utumaji faksi kutoka kwenye kompyuta yoyote, teua Do Not Use.
Bofya OK.
Unaweza kupokea faksi kwenye kompyuta kwa kutumia FAX Utility. Sakinisha FAX Utility kwenye kompyuta ya mteja na uunde mpangilio. Kwa maelezo, tazama Basic Operations kwenye msaada wa FAX Utility (yanayoonyeshwa kwenye dirisha kuu).
Kipengee cha mpangilio kilicho hapa chini kwenye paneli ya udhibiti ya kichapishi kimewekwa kwa Ndiyo, na faksi zilizopokewa zinaweza kuhifadhiwa kwenye kompyuta.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Hifadhi/Sambaza bila masharti > Hifadhi kwenye Kompyuta
Unaweza kuunda mpangilio ili kuchapisha faksi zilizopokewa kwenye kichapishi na pia kuzihifadhi kwenye kompyuta.
Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.
Teua Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Hifadhi/Sambaza bila masharti > Hifadhi kwenye Kompyuta > Ndiyo na Uchapishe.
Ili kuweka kichapishi kutopokea faksi kwenye kompyuta, badilisha mipangilio kwenye kichapishi.
Pia unaweza kubadilisha mipangilio kwa kutumia FAX Utility. Hata hivyo, iwapo kuna faksi zozote ambazo hazijahifadhiwa kwenye kompyuta, kipengele hakifanyi kazi.
Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.
Teua Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Hifadhi/Sambaza bila masharti > Hifadhi kwenye Kompyuta > La.