> Kutuma Faksi > Chaguo za Menyu kwa Kasha la Faksi > Nyaraka Zilizohifadhiwa:

Nyaraka Zilizohifadhiwa:

Unaweza kutafuta Nyaraka Zilizohifadhiwa kwenye Kasha la Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

Unaweza kuhifadhi hadi kurasa 100 za waraka mmoja katika rangi moja, na hadi nyaraka 10 kwenye kikasha. Hii hukuwezesha kuokoa muda uliotumika kutambaza nyaraka wakati unahitaji kutuma waraka huo huo mara kwa mara.

Kumbuka:

Huenda usiweze kuhifadhi nyaraka 10 kulingana na hali ya matumizi kama ukubwa wa nyaraka zilizohifadhiwa.

Nyaraka Zilizohifadhiwa

Huonyesha orodha ya nyaraka zilizohifadhiwa pamoja na tarehe zilipohifadhiwa na kurasa.

Kudonoa mojawapo ya nyaraka zilizohifadhiwa kutoka kwenye orodha huonyesha skrini ya uhakiki. Donoa Anza Kutuma ili kuenda kwenye skrini ya kutuma faksi, au donoa Futa ili kufuta waraka unapohakika.

skrini ya uhakiki
  • : hupunguza au kuongeza.

  • : huzungusha picha upande wa kulia kwa digrii 90.

  • : husogeza skrini katika mwelekeo wa vishale.

  • : husonga kwa ukurasa wa awali au unaofuata.

Ili kuficha ikoni za operesheni, donoa mahali popote kwenye skrini ya uhakiki isipokuwa kwa ikoni. Donoa tena ili kuonyesha ikoni.

(Menyu ya Uhakiki)
  • Hifadhi kwenye Kum'mbu

  • Sambaza(Barua pepe)

  • Tuma mbele(Kabrasha la Mtandao)

  • Chapisha

Wakati ujumbe Futa Ikikamilika unaonyeshwa, teua On ili kufuta faksi baada ya kukamilisha michakato kama vile Hifadhi kwenye Kum'mbu au Sambaza(Barua pepe).

(Menyu ya Kasha)
Hifadhi Data ya Faksi:

Huonyesha skrini kwa kichupo cha Faksi > Mipangilio ya Faksi. Kugusa kwenye skrini huanzisha uchanganuzi wa hati na kuzihifadhi kwenye Nyaraka Zilizohifadhiwa.

Chapisha Zote:

Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huchapisha faksi zote kwenye kikasha. Kuteua On kwenye Futa Ikikamilika hufuta faksi zote wakati uchapishaji umekamilika.

Hifadhi Zote kwenye Kifaa cha Kumbukumbu:

Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huhifadhi faksi zote kwenye vifaa vya kumbukumbu ya nje kwenye kikasha. Kuteua On kwenye Futa Ikikamilika hufuta nyaraka zote wakati kuhifahi kumekamilika.

Futa Zote:

Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Hufuta faksi zote kwenye kikasha.

Mipangilio:

Nywila ya Kufungua Kikasha: unaweza kuweka nywila au kuibadilisha.