Ili kutumia kipengele hiki, hakikisha kwamba programu zifuatazo zimesakinishwa kwenye kompyuta yako.
Epson ScanSmart (Windows 7 au la naadaye, au OS X El Capitan au la baadaye)
Epson Event Manager (Windows Vista/Windows XP, au OS X Yosemite/OS X Mavericks/OS X Mountain Lion/Mac OS X v10.7.x/Mac OS X v10.6.8)
Epson Scan 2 (programu zinazohitajika ili utumie kipengele cha kitambazaji)
Tazama yafuatayo ili uangalie ikiwa kuna programu za kusakinisha.
Windows 10: bofya kitufe cha kuwasha, na kisha ukague kabrasha la Epson Software > Epson ScanSmart, na kabrasha la EPSON > Epson Scan 2.
Windows 8.1/Windows 8: andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
Windows 7: bofya kitufe cha kuwasha kisha uteue Programu Zote. Ifuatayo, angalia kabrasha la Epson Software > Epson ScanSmart, na kabrasha la EPSON > Epson Scan 2.
Windows Vista/Windows XP: bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu. Ifuatayo, angalia kabrasha la Epson Software > Epson Event Manager, na kabrasha la EPSON > Epson Scan 2.
Mac OS: teua Nenda > Programu > Epson Software.
Weka nakala za kwanza.
Teua Changanua > Kompyuta kwenye paneli dhibiti.
Teua kompyuta ya kuhifadhi picha zilizotambazwa.
Unda mipangilio ya utambazaji.
Donoa
.
Unapotumia Windows 7 au la baadaye, au OS X El Capitan au la baadaye: Epson ScanSmart huwashwa kiotomatiki kwenye kompyuta yako, na utambazaji huanza.
Tazama usaidizi wa Epson ScanSmart kwa taarifa kamili ya kutumia programu. Bofya Help kwenye skrini ya Epson ScanSmart ili kufungua msaada.
Huwezi kuanza tu kutambaza kutoka kwenye kichapishi lakini pia kutoka kwenye kompyuta yako kwa kutumia Epson ScanSmart.