Soma maelekezo yafuatayo kabla ya kujaza wino upya.
Weka chupa za wino nje ya mwale wa jua wa moja kwa moja.
Usihifadhi chupa za wino katika halijoto za juu au zinazoganda.
Baada ya kuleta chupa ya wino ndani kutoka eneo baridi la uhifadhi, iwache ipate joto katika halijoto ya chumba kwa angalau saa tatu kabla ya kuitumia.
Pindi unapofungua chupa ya wino, tunapendekeza uitumie haraka iwezekanavyo.
Epson inapendekeza utumie chupa ya wino kabla ya tarehe iliyochapishwa kwenye pakiti.
Usifungue pakiti ya chupa ya wino hadi uwe tayari kujaza tangi la wino.Chupa ya wino hupakiwa bila hewa ili kudumisha utumikaji wake.Ukiwacha chupa ya wino bila kuipakia kwa muda mrefu kabla ya kuitumia, uchapishaji wa kawaida huenda usiwezekane.
Wakati wa kuhifadhi au kusafirisha chupa ya wino, usiinamishe chupa na usiigongeshe au kuiweka mahali penye mabadiliko ya hali joto.La sivyo, wino unaweza kuvuja hata kama kifuniko kilicho kwenye chupa ya wino kimekazwa vizuri.Hakikisha umeweka chupa ya wino ikiwa imesimama wakati unakaza kifuniko, na utahadhari ili uzuie wino usivuje wakati unasafirisha chupa, kwa mfano, kuweka chupa kwenye mkoba.
Wino wa kichapishi hiki unafaa kushughulikiwa kwa uangalifu. Wino unaweza kumwagika wakati matanki ya wino yamejazwa au kujazwa upya na wino. Ikiwa wino utamwagikia nguo au vitu vyako, huenda usitoke.
tumia chupa za wino zilizo na msimbo sahihi wa sehemu ya printa hii.
Usitingishe haraka zaidi au kufinyaza chupa za wino.
Kwa matokeo bora ya kuchapisha usitumie viwango vya wino vilivyo chini kwa vipindi virefu vya muda.
Ili upate matokeo mazuri ya uchapishaji, jaza upya matangi ya wino hadi mstari wa juu angalau mara moja kwa mwaka.
Ili uhakikishe unapokea ubora wa juu wa uchapishaji na kusaidia kulinda kichwa chako ya kuchapisha, akiba tofauti ya usalama ya wino hubakia katika tangi wakati printa yako inakuonyesha unafaa ujaze wino upya.Viwango vilivyoandikwa havijumuishi akiba hii.
Ili kudumisha utendaji mzuri wa kichwa cha kuchapisha, kiasi fulani cha wino hutumiwa kutoka kwenye tanki zote wakati wa operesheni za matengenezo kama vile usafishaji wa kichwa cha kuchapisha. Huenda pia wino ukatumika unapowasha kichapishi.
Wakati unachapisha rangi moja au kijivujivu, wino wa rangu badala ya wino mweusi unaweza kutumiwa kulingana na aina ya karatasi au mipangilio ya ubora wa uchapishaji. Hii ni kwa sababu mchanganyiko wa wino wa rangu unatumiwa kutengeneza rangi nyeusi.
Kiasi fulani cha wino ulio ndani ya chupa za wino ulikuja na printa yako hutumiwa wakati wa usanidi wa mwanzo.Ili uchapishe nakala za hali ya juu, kichwa cha kuchapisha kilicho katika printa yako kitajazwa wino.Mchakato huu wa mara moja hutumia kiasi cha wino na basi chupa hizi zinaweza kuchapisha kurasa chache kulingana na chupa za wino zitakazofuata.
Viwango viliandikwa vinaweza kuwa tofauti kulingana na picha unazochapisha, aina ya karatasi unayotumia, marudio ya uchapishaji na hali ya mazingisa kama vile halijoto.