Haiwezi Kupokea Faksi

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Tunapendekeza uangalie hali ya kichapishi kwenye Hali ya Kazi, iwapo kichapishi kwa sasa kinapokea faksi au la.

KujisaKKujisajili kwenye huduma ya usambazaji wa simu.

Suluhisho

Ikiwa umejisajili kwa huduma ya kusambaza simu, huenda printa isiweze kupokea faksi. Wasiliana na mtoa huduma.

Hii Hali ya Kupokea inawekwa kwa Mwenyewe wakati kifaa cha nje cha simu kimeunganishwa kwenye kichapishi.

Suluhisho

Iwapo kifaa cha simu cha nje kimeunganishwa kwenye kichapishi na kinashiriki laini ya simu na kichapishi, teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi, na kisha uweke Hali ya Kupokea iwe Oto.

Kumbukumbu ya inayopatikana ya kikasha pokezi na kikasha siri haitoshi.

Suluhisho

Nyaraka 100 zilizopokewa zimehifadhiwa kwenye kikasha pokezi na kikasha cha siri kwa jumla. Futa nyaraka zisizofaa.

Kompyuta itaKompyuta itakayohifadhi faksi zilizopokewa haijawashwa.

Suluhisho

Wakati umeunda mipangilio ya kuhifadhi faksi zilizopokewa kwenye kompyuta, washa kompyuta. Faksi iliyopokewa itafutwa pindi tu imehifadhiwa kwenye kompyuta.

Anwani ndogo na nenosiri Anwani ndogo na nywila sio sahihi.

Suluhisho

Unapopokea faksi kutumia kipengele cha anwani ndogo, thibitisha kuwa anwani ndogo na nywila ni sahihi. Thibitisha na mtumaji kuwa anwani ndogo na nywila zinalingana.

Nambari ya faksi ya mtumaji imesajiliwa kwenye Orodha ya Nambari Zilizozuiwa.

Suluhisho

Hakikisha kuwa nambari ya mtyumaji inaweza kufutwa kutoka kwenye Orodha ya Nambari Zilizozuiwa kabla ya kuifuta. Ifute kutoka kwenye Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Faksi ya Kukataliwa > Hariri Orodha ya Nambari Zilizozuiwa. Au lemaza Orodha ya Nambari Zilizozuiwa kwenye Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Faksi ya Kukataliwa > Faksi ya Kukataliwa. Faksi zilizotumwa kutoka kwenye nambari ambazo hazijasajiliwa kwenye orodha hii zimezuiwa wakati mpangilio huu umewezeshwa.

Nambari ya faksi ya mtumaji haijasajiliwa kwenye orodha ya waasiliani.

Suluhisho

Sajili nambari ya faksi ya mtumaji kwenye orodha ya mwasiliani. Au kulemaza Waasiliani Wasiosajiliwa kwenye Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Faksi ya Kukataliwa > Faksi ya Kukataliwa. Faksi zilizotumwa kutoka kwenye nambari ambazo hazijasajiliwa kwenye orodha hii zimezuiwa.

Mtumaji ametuma faksi bila maelezo ya kijajuu.

Suluhisho

Uliza mtumaji iwapo maelezo yamesanidiwa kwenye mashine yake ya faksi. Au, kulemaza Kijajuu cha Faksi kiko Tupu kwenye Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Faksi ya Kukataliwa > Faksi ya Kukataliwa. Faksi ambazo hazijumuishi maelezo ya kijajuu zimezuiwa wakati mpangilio huu umewezeshwa.