> Maelezo ya Msimamizi > Kudhibiti Kichapishi > Kulemaza Kiolesura cha Nje

Kulemaza Kiolesura cha Nje

Unaweza kulemaza kiolesura kinachotumika kuunganisha kifaa kwenye kichapishi. Unda mipangilio ya uzuiaji ili kuzuia uchapishaji na utambazaji kando na kupitia mtandao.

Kumbuka:

Pia unaweza kuunda mipangilio ya uzuiaji kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  • Memory Device: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Kiolesura cha Kifaa cha Kumbukumbu > Kifaa cha Kumbukumbu

  • Muunganisho wa Kompyuta kupitia USB: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Muunganisho wa Kompyuta kupitia USB

  1. Fikia Web Config na uteue Product Security kichupo > External Interface.

  2. Teua Disable kwenye vitendaji unavyotaka kuweka.

    Teua Enable unapotaka kukatisha udhibiti.

    • Memory Device
      Piga marufuku kuhifadhi data kwenye kumbukumbu ya nje kupitia kituo tarishi cha USB kwa muunganisho wa kifaa cha nje.
    • Muunganisho wa Kompyuta kupitia USB
      Unaweza kuzuia matumizi ya muunganisho wa USB kutoka kwenye kompyuta. Iwapo unataka kuizuia, teua Disable.
  3. Bofya OK.

  4. Hakikisha kuwa kituo tarishi kilicholemazwa hakiwezi kutumika.

    • Memory Device
      Thibitisha kuwa hakuna jibu unapounganisha kifaa cha hifadhi kama vile kumbukumbu ya USB kwenye kituo tarishi cha USB ya kiolesura cha nje.
    • Muunganisho wa Kompyuta kupitia USB
      Iwapo kiendeshi kilisakinishwa kwenye kompyuta
      Unganisha kichapishi kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, na kisha uthibitishe kuwa kichapishi hakichapishi na kutambaza.
      Iwapo kiendeshi hakikusakinishwa kwenye kompyuta
      Windows:
      Fungua kidhibiti cha kifaa na ukihifadhi, unganisha kichapishi kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, na kisha uthibitishe kuwa maudhui ya onyesho ya kidhibiti cha kifaa hayabadiliki.
      Mac OS:
      Unganisha kichapishi kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, na kisha uthibitishe kuwa kichapishi hakijaorodheshwa iwapo unataka kuongeza kichapishi kutoka Vichapishi na Vitambazaji.