Mipangilio ya Ripoti

Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Ripoti

Kumbuka:
  • Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.

    Kichupo cha Fax > Report Settings

  • Iwapo ingizo la nywila limeonyeshwa, ingiza nywila.

Kusambaza Ripoti:

Huchapisha ripoti baada ya kusambaza hati ya faski iliyopokewa. Teua Chapisha kuchapisha kila wakati hati inaposambazwa.

Ripoti ya Kosa la Chelezo:

Huchapisha ripoti wakati kosa la chelezo hutokea wakati wa kusambaza faksi iliyotumwa kwa Mfikio wa Chelezo. Unaweza kuweka mipangilio ya eneo katika Faksi > Mipangilio ya Faksi > Chelezo. Kumbuka kwamba kipengele cha chelezo kinapatikana wakati wa:

  • Kutuma faksi kwenye monokromu

  • Kutuma faksi kutumia kipengele cha Tuma Faksi Baadaye

  • Kutuma faksi kutumia kipengele cha Tuma Bechi

  • Kutuma faksi kutumia kipengele cha Hifadhi Data ya Faksi

Chapisha Otomatiki Batli ya Faksi:

Huchapisha logi ya faksi kiotomatiki. Teua Washa(Kila 30) ili kuchapisha kumbukumbu kila kazi 30 za faksi zikikamilika. Chagua Washa(Saa) ili kuchapisha logi wakati uliobainishwa. Hata hivyo, ikiwa idadi ya kazi za faksi imezidi 30, kumbukumbu inachapishwa kabla ya muda uliobainishwa.

Ambatisha Taswira ya Faksi kwenye ripoti:

Huchapisha Ripoti ya Upitishaji pamoja na picha ya ukurawa wa kwanza wa hati iliyotumwa. Teua Washa(Picha Kubwa) ili uchapishe sehemu ya juu ya ukurasa bila kupunguza. Teua Washa(Picha Ndogo) ili kuchapisha ukurasa wote na kuupunguza ili kutoshea kwenye ripoti.

Umbizo la Ripoti:

Huteua umbizo la ripoti za faksi kwenye kichupo cha Faksi > Zaidi > Ripoti ya Faksi kando na Ufuatiliaji Itifaki. Teua Maelezo ili uchapishe pamoja na misimbo ya hitilafu.

Mbinu ya Uingizaji:

Teua mbinu towe ya ripoti za faksi, kama vile Hifadhi kwenye Kum'mbu. Unapoteua Sambaza, teua Mfikio kutoka kwenue waasiliani.