Tahadhari Inayohusiana na Cheti cha Dijitali Hutokea

Ujumbe

Sababu/Jambo la kufanya

Enter a Server Certificate.

Sababu:

Hujateua faili ya kuleta.

Jambo la kufanya:

Teua faili na ubofye Import.

CA Certificate 1 is not entered.

Sababu:

Cheti cha CA 1 hakijaingizwa na Cheti cha CA 2 tu ndicho kimeingizwa.

Jambo la kufanya:

Leta cheti cha CA 1 kwanza.

Invalid value below.

Sababu:

Vibambo visivyoauniwa vimejumuishwa kwenye njia na/au nywila ya faili.

Jambo la kufanya:

Hakikisha kuwa vibambo vimeingizwa sahihi kwa kipengee.

Invalid date and time.

Sababu:

Tarehe na saa ya kichapishi haijawekwa.

Jambo la kufanya:

Weka tarehe na saa kwa kutumia Web Config, EpsonNet Config au paneli dhibiti ya kichapishi.

Invalid password.

Sababu:

Nywila iliyowekwa kwa cheti cha CA na nywila iliyoingizwa haziwiani.

Jambo la kufanya:

Ingiza nywila sahihi.

Invalid file.

Sababu:

Huleti faili ya cheti katika umbizo la X509.

Jambo la kufanya:

Hakikisha kuwa unateua cheti sahihi kilichotumwa na mamlaka ya cheti yanayoaminika.

Sababu:

Faili uliyoleta ni kubwa sana. Ukubwa wa juu wa faili ni 5 KB.

Jambo la kufanya:

Ukiteua faili sahihi, huenda cheti kimeharibika au ni ghushi.

Sababu:

Msururu uliojumuishwa kwenye cheti ni batili.

Jambo la kufanya:

Kwa maelezo zaidi kuhusu cheti, tazama tovuti ya mamlaka ya cheti.

Cannot use the Server Certificates that include more than three CA certificates.

Sababu:

Faili ya cheti katika umbizo la PKCS#12 inajumuisha zaidi ya vyeti 3 vya CA.

Jambo la kufanya:

Leta kila cheti kama kugeuza kutoka umbizo la PKCS#12 hadi umbizo la PEM, au leta gfaili ya cheti katika umbizo la PKCS#12 linalojumuisha hadi vyeti 2 vya CA.

The certificate has expired. Check if the certificate is valid, or check the date and time on your printer.

Sababu:

Cheti kimepitwa na wakati.

Jambo la kufanya:

  • Iwapo cheti kimepitwa na wakati, pata na ulete cheti kipya.

  • Iwapo cheti hakijapitwa na wakati, hakikisha tarehe na saa ya kichapishi imewekwa sahihi.

Private key is required.

Sababu:

Hakuna ufunguo wa kibinafsi uliounganishwa na cheti.

Jambo la kufanya:

  • Iwapo cheti kipo katika umbizo la PEM/DER na kinapatikana kutoka CSR kwa kutumia kompyuta, bainisha faili ya ufunguo wa kibinafsi.

  • Iwapo cheti kipo katika umbizo la PKCS#12 na kinapatikana kutoka CSR kwa kutumia kompyuta, unda faili inayojumuisha ufunguo wa kibinafsi.

Sababu:

Umeleta upya cheti cha PEM/DER kutoka CSR kwa kutumia Web Config.

Jambo la kufanya:

Iwapo cheti kipo katika umbizo la PEM/DER na kinapatikana kutoka CSR kwa kutumia Web Config, unaweza tu kukileta mara moja.

Setup failed.

Sababu:

Haiwezi kukamilisha usanidi kwa sababu mawasiliano kati ya kichapishi na kompyuta yameshindikana au faili haiwezi kusomwa kwa makosa fulani.

Jambo la kufanya:

Baada ya kuangalia faili na mawasiliano yaliyobainishwa, leta tena faili.