Unapowezesha udhibiti wa ufikiaji, mtumiaji tu aliyesajiliwa ataweza kutumia kichapishi.
Fikia Usanidi wa Wavuti na uteue kichupo cha Product Security > Access Control Settings > Basic.
Teua Enables Access Control.
Iwapo utateua Allows printing and scanning without authentication information, unaweza kuchapisha au kutambaza kutoka kwenye viendeshi visivyowekwa kwa maelezo ya uhalalishaji. Iweke unapotaka kudhibiti operesheni tu kutoka kwenye paneli ya udhibiti ya kichapishi na kuruhusu uchapishaji na utambazaji kutoka kwenye kompyuta.
Bofya OK.
Ujumbe wa ukamilisho unaonyeshwa baada ya kipindi fulani cha muda.
Thibitisha kuwa ikoni kama vile nakili na utambaze vimelemazwa kwenye paneli ya udhibiti ya kichapishi.