Wakati nakala au taswira zilizotambazwa ni chafu au zimachakaa, safisha glasi ya kichanganuzi.
Chunga usijibane mkono au vidole wakati unafungua au kufunga kifuniko cha hati. La sivyo unaweza kujeruhiwa.
Usiwahi kutumia pombe au thina kusafisha printa. Kemikali hizi zinaweza kuharibu printa.
Fungua kifuniko cha hati.

Tumia kitambaa laini, safi na kikavu kusafisha glasi ya kichanganuzi.
Iwapo eneo la kioo limekwamiliwa na grisi au nyenzo nyingine ngumu kuondoa, tumia kiasi kidogo cha kisafishaji kioo na kitambaa laini kuiondoa. Pangusa unyevu wote unaobakia.
Usibonyeze glasi kwa nguvu.
Kuwa makini usikwaruze au kuharibu glasi. Glasi iliyoharibika inaweza kupunguza ubora wa utambazaji.