Kukatisha Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi)

Kuna mbinu mbili zinazopatikana za kulemaza muuganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi); unaweza kulemaza miunganisho yote kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, au kulemaza kila muunganisho kutoka kwenye kompyuta au kifaa maizi. Unapotaka kulemaza miunganisho yote, angalia kiungo cha maelezo husiani kilicho hapa chini kwa maelezo.

Muhimu:

Wakati muunganisho wa Wi-Fi Direct wa (AP Rahisi) unalemazwa, kompyuta zote na vifaa maizi vilivyounganishwa kwenye kichapishi katika muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) vinatenganishwa.

Kumbuka:

Iwapo unataka kukata muunganisho wa kifaa maalum, kata muunganisho kutoka kwenye kifaa badala ya kichapishi. Tumia mojawapo ya mbinu zifuatazo ili kukata muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) kutoka kwenye kifaa.

  • Kata muunganisho wa Wi-Fi kwenye jina la mtandao la kichapishi (SSID).

  • Unganisha kwenye jina jingine la mtandao (SSID).