Usimamizi wa Mtandao

Kwa kutumia menyu hii, unaweza kudumisha bidhaa kama msimamizi wa mfumo. Pia hukuruhusu kuzuia vipengele vya bidhaa kwa watumiaji binafsi ili kukidhi kazi yako au mtindo wa ofisi.

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao

Kisimamia Waasiliani:

Unaweza kuunda mipangilio inayofuata kwa waasiliani.

Sajili/Futa:

Sajili na/au futa waasiliani kwa menyu ya Faksi, Kwenye Kompyuta (Barua pepe), na Changanua kwa Folda/FTP ya Mtandao.

Mara kwa mara:

Sajili waasiliani wanaotumiwa mara kwa mara ili kuwafikia haraka. Pia unaweza kubadilisha mpangilio wa orodha.

Chapisha Waasiliani:

Chapisha anwani yako ya orodha.

Angalia Chaguo:

Badilisha jinsi orodha ya waasiliani inavyoonyeshwa.

Chaguo za Utafutaji:

Badilisha mbinu ya kutafuta waasiliani.

Ondoa Data ya Kumbukumbu ya Ndani:

Futa data ya kumbukumbu ya ndani ya kichapishi, kama vile kazi na manenosiri.

Mipangilio ya Usalama:

Unaweza kuunda mipangilio ya usalama ifuatayo.

Vikwazo:

Toa kibali cha kubadilisha mipangilio ya vipengee vifuatavyo wakati kufuli la paneli limewezeshwa.

  • Ufikiaji wa kumbukumbu ya Kazi

  • Fikia ili uweze Kuwasajili/Kuwafuta Waasiliani

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Faksi

  • Ufikiaji wa Batli ya Usambazaji Faksi

  • Ufikiaji wa Ripoti ya Faksi

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Kuh. Cha. kwa Folda/FTP ya Mt'o

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Changanua kwa Barua pepe

  • Ufikiaji wa Onyesha Historia ya Zil'tumwa ya Cha. Barua pepe

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Zil'tumwa ya Cha. Barua pepe

  • Ufikiaji wa Lugha

  • Ufikiaji wa Karatasi Nyembamba

  • Ufikiaji wa Hali Tulivu

  • Ulinzi wa Data ya Kibinafsi

Fikia Vidhibiti:

Teua On ili kuzuia vipengele vya bidhaa. Hii huwahitaji watumiaji kuingia kwenye paneli dhibiti ya bidhaa kwa majina yao ya mtumiaji na nenosiri kabla waweze kutumia vipengele vya paneli dhibiti. Kwenye Kubali Kazi za Mtumiaji Asiyejulikana, unaweza kuteua iwapo utaruhusu kazi zisizo na maelezo yanayostahili ya uhalalishaji au la.

Mipangilio ya Msimamizi:
  • Nenosiri la Msimamizi

    Weka, badilisha, au ufute nenosiri la msimamizi.

  • Mpangilio wa Kufunga

    Teua kama utafunga paneli dhibiti au la kwa kutumia nenosiri lililosajiliwa katika Nenosiri la Msimamizi.

Ufichamishaji wa Nenosiri:

Teua On ili kusimba nywila yako kwa njia fiche. Ukibonyeza kitufe cha kuzima wakati kinaendelea kuanzisha upya, data inaweza kuharibiwa na mipangilio ya kichapishi kurejeshwa kuwa chaguomsingi. Katika hali hiyo, weka tena maelezo ya nywila.

Utafiti wa Wateja:

Teua Idhinisha ili kutoa maelezo ya matumizi ya bidhaa kama vile idadi ya machapisho kwa Seiko Epson Corporation.

Rejeza Mipangilio Chaguo-msingi:

Weka upya mipangilio kwenye menyu zifuatazo katika changuo-msingi zake.

  • Mipangilio ya Mtandao

  • Nakili Mipangilio

  • Mip'o ya Ucha'uzi

  • Mipangilio ya Faksi

  • Ondoa Data na Mipangilio Yote

Sasisho la Pro.:

Unaweza kupata maelezo ya programu dhibiti kama vile toleo lako la sasa na maelezo kuhusu visasisho vinavyopatikana.

Sasisha:

Angalia iwapo toleo la sasa la programu dhibiti imepakiwa kwenye seva ya mtandao.Iwapo kisasisho kinapatikana, unaweza kuteua iwapo utaanza kusasisha au la.

Taarifa:

Teua On ili kupokea taarifa iwapo kisasisho cha programu dhibiti inapatikana.