> Kunakili > Mbinu Zinazopatikana za Kunakili > Kunakili Nakala asili Anuwai kwenye Laha Moja

Kunakili Nakala asili Anuwai kwenye Laha Moja

Unaweza kunakili nakala asili anuwai kwenye laha moja la karatasi.

  1. Weka nakala zote asili zikiwa zinaangalia juu katika ADF.

    Ziweke katika mwelekeo ulioonyeshwa kwenye mfano.

    • Mwelekeo wa kusomeka
    • Mwelekeo wa Kushoto
    Muhimu:

    Iwapo unataka kunakili nakala asili ambazo haziauniwi na ADF, tumia glasi ya kitambazaji.

    Nakala asili ambazo Haziauniwi na ADF

    Kumbuka:

    Pia unaweza kuweka nakala asili kwenye glasi ya kitambazaji.

    Kuweka Nakala Asili

  2. Teua Nakili kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Teua kichupo cha Mahiri, teua Kurasa Nyingi, kisha uteua 2-juu au 4-juu.

  4. Bainisha mpangilio wa muundo na mwelekeo asili.

  5. Donoa .