Huchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli ili kuangalia iwapo nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.
Husafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha. Kwa sababu kipengele hiki hutumia wino kidogo, safisha kichwa cha kuchapisha tu iwapo baadhi ya nozeli zimeziba kama ilivyoonyeshwa kwenye mfano wa ruwaza ya kukagua nozeli.

Huendesha usafishaji wa nishati wa nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha. Kwa sababu kipengele hiki hutumia wino zaidi kulinga usafishaji wa kichwa, endesha usafishaji wa nishati tu iwapo nozeli nyingi zimeziba kama ilivyoonyeshwa kwenye mfano wa ruwaza ya kukagua nozeli.

Hufungua dirisha la Laiti ya Kipangaji cha Kazi. Hapa unaweza kufungua na kuhariri data iliyohifadhiwa awali.
Hufungua dirisha la EPSON Status Monitor 3. Unaweza kuthibitisha hali ya kichapishi na matumizi yake hapa.
Hukuruhusu kuunda mipangilio kwa vipengee kwenye dirisha la EPSON Status Monitor 3.
Hukuruhusu kuunda mipangilio mbalimbali. Bofya kulia kila kipengee ili kuona Msaada kwa maelezo zaidi.
Huonyesha kazi zinazosubiri kuchapishwa. Unaweza kuangalia, kusitisha, au kuendelea na kazi za kuchapisha.
Huonyesha idadi ya laha za karatasi zilizoingizwa kwenye kichapishi au ADF.
Hubadilisha lugha ya kutumiwa kwenye dirisha la kiendeshi cha kichapishi. Ili kutekeleza mipangilio, funga kiendeshi cha kichapishi, na kisha ukifungue tena.