Kuunganisha kwenye Ethaneti

Unganisha kichapishi kwenye mtandao kwa kutumia kebo ya Ethaneti, na uangalie muunganisho.

  1. Unganisha kichapishi na kitovu (swichi ya LAN) kwa kebo ya Ethaneti.

  2. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho.

    Matokeo ya uchunguzi wa muunganisho yanaonyeshwa. Thibitisha muunganisho ni sahihi.

  4. Donoa Sawa ili kukamilisha.

    Unapodonoa Chapisha Ripoti ya Ukaguzi, unaweza kuchapisha matokeo ya uchunguzi. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuichapisha.