> Hoja za Kufurahisha za Kuchapisha > Kuchapisha Mabango ya Utafiti, Vibandiko vya Jina, au Kadi za Alfabeti

Kuchapisha Mabango ya Utafiti, Vibandiko vya Jina, au Kadi za Alfabeti

Sehemu hii inafafanua jinsi ya kuchapisha mabango ya utafiti, vibandiko vya jina, au kadi za alfabeti kwa kutumia programu ya kompyuta ya Epson Photo+. Unapochapisha kadi za alfabeti, tunapendekeza kuchapisha kwenye karatasi nzito.

  1. Anzisha Epson Photo+.

    Programu ya Uchapishaji Haraka na Furaha kutoka katika Kompyuta (Epson Photo+)

  2. Bofya Free Layout.

  3. Teua ukubwa wa karatasi na mwelekeo, na kisha ubofye OK.

  4. Bofya , na kisha uteue rangi au ruwaza ya mandhirinyuma.

  5. Bofya , na kisha uweke matini kwenye kikasha cha matini.

  6. Kwenye Edit Text, hariri fonti, uubwa, na rangi ya matini.

  7. Bofya , na kisha uteue mihuri.

    Kumbuka:

    Pia unaweza kuongeza picha kwa kubofya .

  8. Teua aina ya karatasi unayotaka kuchapisha kutoka kwenye mpangilio wa Media Type.

  9. Weka vipengele hivyo vingine inavyohitajika.

  10. Pakia karatasi katika kichapishi na uanze kuchapisha.