Ikiwa kesi ya nje ya kichapishi ni chafu au ina vumbi, zima kichapishi na uisafishe kwa kutumia nguo laini, safi na yenye unyevunyevu. Ikiwa huwezi kuondoa uchafu, jaribu kusafisha kwa kutumia nguo laini, safi na yenye unyevunyevu uliowekwa kwa kutumia sabuni kolezi.

Kuwa makini ili usimwage maji ndani ya mtambo wa kichapishi au viambajengo vyake vya kielektroniki. La sivyo, kichapishi kinaweza kuharikibika.
Usitumia pombe au kiyeyusha rangi kusafisha kifuniko cha kichapishi. Kemikali hizi zinaweza kuharibu viambajengo na kesi.
Usiguze kebo nyeupe bapa, sehemu angavu, na tyubu za wino zilizo ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.
