Tayarisha mapema data yako ya chapisho. Sehemu hii inafafanua jinsi ya kuchapisha kwa kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson.
Tunapendekeza kuchapisha kwenye karatasi nzito.

Fungua data ya kuchapisha uliyotayarisha na ufikie dirisha la kichapishi kutoka kwenye menyu ya kuchapisha.
Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi cha Kuu, teua aina ya karatasi unalotaka kuchapisha kutoka kwenye mpangilio wa Aina ya Krtasi.
Unapotaka kuunda machapisho ya pande 2, teua Otomatiki (Kujalidi ukingo mrefu) au Otomatiki (Kujalidi ukingo mfupi) kutoka kwenye mpangilio wa Uchapishaji wa Pande 2.
Weka vipengele hivyo vingine inavyohitajika.
Pakia karatasi katika kichapishi na uanze kuchapisha.