Mbinu hii hukuruhusu kuunganisha kichapishi moja kwa moja kwenye vifaa maizi bila kipanga njia pasiwaya.
Unahitaji kuunda mipangilio hii kwa kichapishi na kifaa maizi unachotaka kuunganisha mara moja. Isipokuwa ulemaze Wi-Fi Direct au kurejesha mipangilio ya mtandao kwa chaguo-msingi yake, huhitaji kuunda mipangilio hii tena.
Donoa
kwenye skrini ya nyumbani.
Donoa Wi-Fi Direct.
Donoa Anza Kusanidi.
Donoa Vifaa Vingine vya OS.

Jina la Mtandao(SSID) na Nenosiri kwa Wi-Fi Direct vya kichapishi vinaonyeshwa.
Kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi, teua SSID iliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti, na kisha uingize nenosiri.

Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua Ifuatayo.
Kwenye kifaa maizi, washa programu ya uchapishaji ya Epson.
Mifano ya programu za uchapishaji za Epson

Kwenye skrini ya programu ya uchapishaji ya Epson, donoa Printer is not selected.
Teua kichapishi unachotaka kuunganisha.

Tazama maelezo yaliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi ili kuteua kichapishi.

Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua Imekamilika.
Kwa vifaa maizi ambavyo vimeunganishwa kwenye kichapishi mbeleni, teua jina la mtandao (SSID) kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi ili kuviunganisha tena.