Suluhisho
Unapochapisha kwenye karatasi tupu, lemaza mpangilio wa uchapishaji wa pande mbili.
Wakati wa uchapishaji wa pande mbili (au kasi ya juu), kichwa cha kuchapisha huchapisha kikisogea pande zote mbili, na mistari wima huenda ikakosa kulingana. Kulemaza mipangilio huenda kukapunguza kasi ya uchapishaji lakini kukaimarisha ubora wa chapisho.
Paneli Dhibiti
Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa, na kisha ulemaze Mwelekeo.
Windows
Futa Uchapishaji katika mielekeo miwili iliyo kwenye kichupo cha kiendesha kichapishi cha Chaguo Zaidi.
Mac OS
Teua Mapendeleo ya Mfumo kwenye menyu ya Apple > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi), na kisha uteue kichapishi. Bofya Chaguo na Vifaa > Chaguo (au Kiendeshi). Teua Off kama mpangilio wa High Speed Printing.
Suluhisho
Unapochapisha kwenye karatasi ya picha, chapisha kwa kutumia mpangilio wa ubora wa juu.
Paneli Dhibiti
Teua Bora kama Ubora kwenye kichupo cha Mahiri katika mipangilio ya uchapishaji.
Windows
Teua Juu kutoka Ubora kwenye kichapishi cha kichupo cha Kuu.
Mac OS
Teua Nzuri kama Print Quality kutoka kwenye menyu ya kidirisha cha Mipangilio ya Kuchapisha.