EPSON Software Updater ni programu ambayo husakinisha programu mpya na kusasisha vifaa dhabiti na miongozo kupitia Mtandao.
Programu endeshi za Windows Server hazikubaliwi.
Windows 10
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Epson Software > EPSON Software Updater.
Windows 8.1/Windows 8
Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
Windows 7/Windows Vista/Windows XP
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote (au Programu) > Epson Software > EPSON Software Updater.
Kadhalika, unaweza kuwasha EPSON Software Updater kwa kubofya ikoni ya kichapishi kwenye mwambaa kazi ulio kwenye eneo kazi, na kisha uteue Kisasisho cha Programu.
Teua Nenda > Programu > Epson Software > EPSON Software Updater.