Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Huwezi kubadilisha mipangilio iliyozuiwa na msimamizi wako.
Rekebisha sauti.
Nyamazisha
Teua On ili kunyamazisha sauti.
Hali ya Kawaida
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe.
Hali Tulivu
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe kwenye Hali Tulivu.
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Chagua Washa urudi kwenye modi ya kulala (modi ya kuhifadhi nishati) kwa kugusa paneli ya mguso. Wakati imezimwa unahitaji kubonyeza kitufe kilicho kwenye paneli dhibiti ili uamshe printa. Kuzima kipengele hiki huzuia utendaji wowote usiokusudiwa kutokea kwa sababu ya vitu vya kigeni vinavyogusa skrini. Pia unaweza kuweka kipindi cha muda ambao kupengee hiki kimewasha.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha LINE kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Angalia tovuti ifuatayo kwa muda maalum.
Tarehe/Saa
Ingiza tarehe na saa ya sasa.
Saa za Mchana Mrefu
Teua mpangilio wa wakati wa majira ya joto unaotumika katika eneo lako.
Utofauti wa Saa
Ingiza tofauti ya saa kati ya saa yako ya ndani na UTC (Saa Inayoratibiwa ya Kimataifa).
Teua nchi au eneo ambalo unatumia kichapishi chako. Iwapo utabadilisha nchi au eneo, mipangilio yako ya faksi inarejea kwa chaguo-msingi na lazima uiteue tena.
Bainisha menyu ya kwanza inayoonyeshwa kwenye skrini ya LCD wakati kichapishi kinawaka na Muda wa Shughuli Umeisha imewezeshwa.
Badillisha muundo wa ikoni kwenye skrini ya LCD. Pia unaweza kuongeza, kuonmdoa, na kuhamisha ikoni.