Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza
Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.
Fax kichupo > Save/Forward Settings > Conditional Save/Forward
Unaweza kuweka mafikio ya kuhifadhi na/au kutuma mbele kwenye Kisanduku pokezi, vikasha vya siri, kifaa cha kumbukumbu ya nje, anwani za barua pepe, makabrasha yaliyoshirikiwa, na mashine mengine ya faksi.
Ili kubadili kati ya kuwezesha au kulemaza masharti, donoa mahali popote kwenye kipengee kilichowekwa isipokuwa kwa
.
Teua masharti na uweke mipangilio.
Nambari ya faksi ya mtumaji inapofanana, faksi iliyopokewa inahifadhiwa na kusambazwa.
Anwani ndogo (SUB) zinapofanana kikamilifu, faksi iliyopokewa inahifadhiwa na kusambazwa.
Nenosiri (SID) linafanana kikamlifu, faksi iliyopokewa inahifadhiwa na kusambazwa.
Huhifadhi na kusambaza faksi iliyopokewa wakati wa kipindi cha muda kilichobainishwa.
Teua mafikio ili kuhifadhi na kutuma mbele nyaraka zilizopokewa zinazolingana na masharti. Unaweza kutumia vipengele vilivyo hapa chini kwa wakati mmoja.
Huhifadhi faksi zilizopokelewa kwenye Kisanduku pokezi cha kichapishi au kisanduku cha siri.
Unaweza kuhifadhi hadi juimla ya nyaraka 100. Kumbuka kuwa kuhifadhi nyaraka 100 kunaweza kuwa vigumu kulingana na masharti ya matumizi kama vile ukubwa wa faili za nyaraka zilizohifadhiwa, na kutumia vipengele mbalimbali vya kuhifadhi faksi kwa wakati mmoja.
Huhifadhi faksi zilizopokewa kama faili za PDF kwenye kifaa cha kumbukumbu ya nje kilichounganishwa kwenye kichapishi.
Hati zilizopokewa uhifadhiwa kwa muda kwenye kumbukumbu ya kichapishi kabla ya nyaraka kuhifadhiwa kwenye kifaa cha kumbukumbu kilichounganishwa kwenye kichapishi. Kwa sababu hitilafu ya kumbukumbu kujaa hulemaza kutuma na kupokea faksi, weka kifaa cha kumbukumbu kikiwa kimeunganishwa kwenye kichapishi.
Hutuma mbele faksi zilizopokewa kwenye mashine mengine ya faksi, au kuzituma mbele kama faili za PDF kwenye kabrasha lililoshirikiwa kwenye mtandao au kwa anwani ya barua pepe. Faksi zilizotumwa mbele hufutwa kwenye kichapishi. Kwanza ongeza mafikio ya utumaji mbele kwenye orodha ya waasiliani. Ili kusambaza kwa anwani ya barua pepe, unahitaji pia kusanidi mipangilio ya seva ya barua pepe.
Mfikio: unaweza kuteua mafikio ya utumaji mbele kutoka kwenye orodha ya waasiliani uliyoiongeza mapema.
Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao au anwani ya barua pepe kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha iliyochanganuliwa hadi kwa mwishilio katika hali ya uchanganuzi. Teua Changanua > Barua pepe, au Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye skrini ya nyumbani, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.
Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana: unaweza kuteua iwapo utachapisha faksi iliyoshindikana au kuihifadhi kwenye Kisanduku pokezi.
Hutuma taarifa ya barua pepe wakati mchakato uliouteua hapa chini umekamilika. Unaweza kutumia vipengele vilivyo hapa chini kwa wakati mmoja.
Weka mafikio ya taarifa ya ukamilishaji wa mchakato.
Hutuma taarifa wakati upokeaji wa faksi umekamilika.
Hutuma taarifa wakati uchapishaji wa faksi umekamilika.
Hutuma taarifa wakati kuhifadhi faksi kwenye kifaa cha kumbukumbu kumekamilika.
Hutuma taarifa wakati usambazaji wa faksi umekamilika.