> Kunakili > Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili

Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Kurasa Nyingi:

Teua muundo wa nakala.

  • Ukurasa Mmoja

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.

  • 2-juu

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.

  • 4-juu

    Hunakili hati halisi zenye pande nne kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 4-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.

Ukubwa Asili:

Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza. Unaponakili nakala asili za ukubwa usio wastani, teua ukubwa unaokaribiana na nakala yako asili.

Kumalizia:

Teua jinsi ya kuondoa karatasi kwa nakala anuwai za hati halisi anuwai.

  • Kikundi (Kurasa Sawa)

    Hunakili nakala asili kwa ukurasa kama kikundi.

  • Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa)

    Huchapisha nakala nyingi za hati nyingi halisi zilizolinganishwa kimpangilio na kupangwa kwenye vikundi.

Mwelekeo (Asili):

Teua mwelekeo wa nakala yako asili.

Ubora wa Taswira:

Rekebisha mipangilio ya taswira.

  • Ulinganuzi

    Rekebisha tofauti kati ya mwangaza na sehemu za giza.

  • Kulowesha

    Rekebisha udhahiri wa rangi.

  • Uwiano Mwekundu, Uwiano wa Kijani, Uwiano wa Bluu

    Rekebisha wiani wa kila rangi.

  • Ukali

    Rekebisha ufupisho wa taswira.

  • Udhibiti wa Rangi

    Rekebisha toni ya rangi ya ngozi. Donoa + ili kuifanya baridi (kuongeza kijani) na udonoe - ili kuifanya joto (ongeza nyekundu).

  • Ondoa Mand'yuma

    Rekebisha wiani wa rangi ya mandharinyuma. Donoa + ili kuifanya ng’avu (nyeupe) na udonoe - ili kuifanya kolevu (nyeusi).

Pambizo ya Kufunga:

Teua kama vile eneo la uunganishaji, kingo na mwelekeo wa nakala yako asili.

Pu. ili Itoshee Kar'i:

Hunakili picha zilizotambazwa kwa ukubwa mdogo kuliko thamani ya Pung/Ong'a ili kutoshea ndani ya ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Pung/Ong'a ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.

Ondoa Kivuli:

Huondoa vivuli vinavyoonekana kwenye nakala unaponakili karatasi nzito au vinavyotokea katikati ya nakala unaponakili kijitabu.

Ond. Mas'o ya Panchi:

Huondoa mashino ya kufunga wakati wa kunakili.

Nakala ya Kadi ya ID:

Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi.