> Maelezo ya Msimamizi > MMipangilio ya Kutumia Kichapishi > Kusanidi Seva ya Barua > Vipengee vya Mpangilio wa Seva ya Barua

Vipengee vya Mpangilio wa Seva ya Barua

Vipengele

Mipangilio na Ufafanuzi

Authentication Method

Bainisha mbinu ya uhalalishaji kwa kichapishi ili kufikia seva ya barua.

Off

Weka wakati seva ya barua haihitaji uhalalishaji.

SMTP AUTH

Huhalalishwa kwenye seva ya SMTP (seva ya barua inayoondoka) unapotuma barua pepe. Seva ya barua inahitaji kuauni uhalalishaji wa SMTP.

POP before SMTP

Huhalalisha kwenye seva ya POP3 (seva ya kupokea barua) kabla ya kutuma barua pepe. Unapoteua kipengee hiki, weka seva ya POP3.

Authenticated Account

Ukiteua SMTP AUTH au POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza jina la akaunti ya uhalalishaji kati ya vibambo 0 na 255 kwenye ASCII (0x20–0x7E).

Unapoteua SMTP AUTH, ingiza akaunti ya seva ya SMTP. Unapoteua POP before SMTP, ingiza akaunti ya seva ya POP3.

Authenticated Password

Iwapo utateua SMTP AUTH au POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza nenosiri lililohalalishwa kati ya vibambo 0 na 20 kwenye ASCII (0x20–0x7E).

Unapoteua SMTP AUTH, ingiza akaunti iliyohalalishwa kwa seva ya SMTP. Unapoteua POP before SMTP, ingiza akaunti iliyohalalishwa kwa seva ya POP3.

Sender's Email Address

Ingiza anwani ya barua pepe ya mtumaji kama vile anwani ya barua pepe ya msimamizi wa mfumo. Hii inatumika unapohalalisha, kwa hivyo ingiza anwani halali ya barua pepe iliyosajiliwa kwenye seva ya barua.

Ingiza kati ya vibambo 0 na 255 kwenye ASCII (0x20–0x7E) isipokuwa kwa : ( ) < > [ ] ; ¥. Kitone “.” hakiwezi kuwa kibambo cha kwanza.

SMTP Server Address

Ingiza vibambo kati ya 0 na 255 kwa kutumia A–Z a–z 0–9 . -. Unaweza kutumia umbizo la IPv4 au FQDN.

SMTP Server Port Number

Ingiza nambari kati ya 1 na 65535.

Secure Connection

Teua mbinu ya usimbaji fiche wa mawasiliano kwenye seva ya barua.

None

Iwapo utateua POP before SMTP kwenye Authentication Method, muunganisho haujasimbwa fiche.

SSL/TLS

Hii inapatikana wakati Authentication Method imewekwa kwa Off au SMTP AUTH. Mawasiliano yanasimbwa fiche kutoka mwanzo.

STARTTLS

Hii inapatikana wakati Authentication Method imewekwa kwa Off au SMTP AUTH. Mawasilano hayasimbwi fiche kutoka mwanzo, lakini kulingana na mazingira ya mtandao, iwapo mawasiliano yamesimbwa fiche au la yanabadilishwa.

Certificate Validation

Cheti kinahalalishwa hii inapowezeshwa. Tunapendekeza hii iwekwe kwa Enable. Ili kusanidi, unahitaji kuleta CA Certificate kwenye kichapishi.

POP3 Server Address

Ukiteua POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza anwani ya seva ya POP3 kati ya vibambo 0 na 255 kwa kutumia A–Z a–z 0–9 . -. Unaweza kutumia umbizo la IPv4 au FQDN.

POP3 Server Port Number

Ukiteua POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza nambari ya kati ya 1 na 65535.