Vipengee Vinavyoweza Kuwekwa Kibinafsi

Msimamizi anaweza kuruhusu vipengee kuonyeshwa na kubadilisha mipangilio kibinafsi.

  • Ufikiaji wa kumbukumbu ya Kazi: Hali ya Kazi > Kumbukumbu

    Dhibiti onyesho la hali ya historia ya kazi ya kiwambo. Teua On ili kuruhusu historia ya kazi kuonyeshwa.

  • Fikia ili uweze Kuwasajili/Kuwafuta Waasiliani: Mipangilio > Kisimamia Waasiliani > Sajili/Futa

    Dhibiti usajili na kubadilika kwa waasiliani. Teua On ili kusajili au kubadilisha waasiliani.

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Faksi: Faksi > Mpokeaji > Hivi karibuni

    Dhibiti onyesho la mafikio unapotuma na kupokea faksi. Teua On ili kuonyesha mafikio.

  • Ufikiaji wa Batli ya Usambazaji Faksi: Faksi > Menyu > Kumbukumbu ya Upitishaji

    Dhibiti onyesho la historia ya mawasiliano ya faksi. Teua On ili kuonyesha historia ya mawasiliano.

  • Ufikiaji wa Ripoti ya Faksi: Faksi > Menyu > Ripoti ya Faksi

    Dhibiti uchapishaji wa ripoti ya faksi. Teua On ili kuruhusu uchapishaji.

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Kuh. Cha. kwa Folda/FTP ya Mt'o: Changanua > Folda/FTP ya Mtandao > Menyu > Chapisha Historia ya Kuhifadhi

    Dhibiti uchapishaji wa historia ya kuhifadhi kwa kutambaza kwenye kitendaji cha kabrasha la mtandao. Teua On ili kuruhusu uchapishaji.

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Changanua kwa Barua pepe: Changanua > Barua pepe > Mpokeaji > Historia

    Dhibiti onyesho la historia kwa kutambaza kwenye kitendaji cha barua. Teua On ili kuonyesha historia.

  • Ufikiaji wa Onyesha Historia ya Zil'tumwa ya Cha. Barua pepe: Changanua > Barua pepe > Menyu > Onyesha Historia ya Kutuma

    Dhibiti onyesho la historia ya kutuma barua pepe kwa kutambaza kwenye kitendaji cha barua. Teua On ili kuonyesha historia ya kutuma barua pepe.

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Zil'tumwa ya Cha. Barua pepe: Changanua > Barua pepe > Menyu > Chapisha Historia ya Kutuma

    Dhibiti uchapishaji wa historia ya kutuma barua pepe kwa kutambaza kwenye kitendaji cha barua. Teua On ili kuruhusu uchapishaji.

  • Ufikiaji wa Lugha: Mipangilio > Lugha/Language

    Dhibiti mabadiliko ya lugha inayoonyeshwa kwenye paneli dhibiti. Teua On ili kubadilisha lugha.

  • Ufikiaji wa Karatasi Nyembamba: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Karatasi Nyembamba

    Dhibiti mabadiliko ya mipangilio ya kitendaji cha Karatasi Nyembamba. Teua On ili kubadilisha mipangilio.

  • Ufikiaji wa Hali Tulivu: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Hali Tulivu

    Dhibiti mabadiliko ya mipangilio ya kitendaji cha Hali Tulivu. Teua On ili kubadilisha mipangilio.

  • Ulinzi wa Data ya Kibinafsi:

    Dhibiti onyesho la maelezo ya mafikio kwenye usajili wa upigaji haraka. Teua On ili kuonyesha mafikio kama (***).