Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa:
Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.
Teua chanzo cha karatasi ambacho karatasi huingizwa. Teua Uteuzi Otomatiki ili kuteua kiotomatiki chanzo cha karatasi kilichoteuliwa kwenye mipangilio ya kichapishi.
Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo utateua Mtumiaji-Amefafanuliwa, ingiza upana na urefu wa karatasi.
Hukuzwa kiasi kidogo zaidi ya ukubwa wa karatasi ili kusiwe na pambizo zinachapishwa kando ya kingo za karatasi. Bofya Mipangilio ili uteue kiwango cha ukuzaji.
Teua ubora wa chapisho unaotaka kutumia kwa uchapishaji. Mipangilio inayopatikana inalinganana aina ya karatasi unayoteua. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.
Hukuruhusu kutekeleza uchapishaji wa pande 2.
Unaweza kubainisha ukingo wa kuunganisha na pambizo za kuunganisha. Unapochapisha nyaraka za kurasa nyingi, unaweza kuteua kuchapisha kuanzia upande wa mbele au upande wa nyuma wa ukurasa.
Teua aina ya waraka ili kurekebisha uzito wa chapisho. Iwapo uzito wa chapisho unaofaa umeteuliwa, unaweza kuzuia picha kutokea upande wa nyuma. Teua User Defined ili kurekebisha uzito wa chapisho kikuli.
Hukuruhusu kuchapisha kurasa nyingi kwenye laha moja au kutekeleza uchapishaji wa bango. Bofya mpangilio wa muundo ili kubainisha utaratibu ambao kurasa zinachapishwa.
Weka idadi ya nakala unazotaka kuchapisha.
Huchapisha nyaraka nyingi zilizolinganishwa kwa utaratibu na kupangwa kwenye vikundi.
Hukuruhusu kuchapisha kutoka ukurasa wa mwisho ili kurasa zikusanywe kulingana na mpangilio sahihi baada ya kuchapisha.
Hupunguza kelele ambayo kicvhapishi hutoa. Hata hivyo, uwezeshaji wa hii unaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Kipengele cha Job Arranger Lite hukuruhusu kujumuisha faili mbalimbali zilizoundwa na programu tofuti na uzichapishe kama kazi moja ya uchapishaji.
Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.